Bondia Tyson Fury na Oleksandr Usyk ambao walizichapa wiki chache zilizopita wanatarajia kupanda tena ulingoni Desema 21, 2024.
Taarifa ya pambano hilo imethibitishwa leo Mei 29, 2024 na mwenyekiti wa mamlaka za burudani kutoka Riyadh, nchini Saudi Arabia, Turki Alalshikh ambapo pambano hilo linatarajiwa kufanyika.
Ikumbukwe kuwa pambano la kwanza lilifanyika Mei 18 2024, huku Usyk akimchapa Fury na kujipatia rekodi ya ‘Undisputed Champion’ iliyokuwa ikishikiriwa na Lennox Lewis mwaka 1999 na kuondoka na mikanda minne ya masumbwi IBF, WBO,WBA na WBC.
Aidha kwa mujibu wa promota wa Fury, Fank Warren ameweka wazi kuwa mabondia hao walisaini mkataba wa pambano la marudiano kabla ya pambano la kwanza, huku akitupa karata yake kwa Tyson Fury akiamini kuwa bondia huyo atashinda.
Leave a Reply