Baada ya kutangaza kupata changamoto ya kiafya kwenye ndege, bondia wa uzani wa juu Mike Tyson, amewaondoa hofu mashabiki wake kwa kueleza kuwa kwa sasa yupo sawa asilimia 100.
#Tyson kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa anajihisi yupo sawa kwa asilimia 100 lakini ahitaji kumpiga Jake Paul.
#Tyson anatarajia kuingia ulingoni na #JakePaul Julai 20, 2024 katika uwanja wa AT&T, pia pambano hilo litaoneshwa moja kwa moja (live) katika mtandao wa #Netflix.
Ikumbukwe kuwa siku mbili zilizopita #MikeTyson, alipata dharura ya kiafya ndani ya ndege na kupatiwa matibabu humo humo akiwa anatoka Miami kuelekea Los Angeles.

Leave a Reply