Tyrese: Ex wangu alifata pesa na umaarufu

Tyrese: Ex wangu alifata pesa na umaarufu

Aloo!! Kumbe utapeli katika mapenzi bado tatizo kubwa, sasa bwana muigizaji kutoka nchini Marekani Tyrese Gibson kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema kuwa amekuja kugundua kuwa aliyekuwa mke wake Samantha Lee alikuwa naye kwenye ndoa sababu ya pesa na umaarufu alikuwa nao na sio upendo.

Kwenye video alisikika akisema "Mimi ndiye niliyekuwa muigizaji kwenye mahusiano yetu lakini nikaja kugundua kumbe nilikuwa na mahusiano miaka 5 na mmoja ya waigizaji bora niliowahi kuwaona kwenye maisha yangu”alisema Tyrese Gibson.

Tyrese anasema amegundua hilo katika kipindi cha mchakato wa talaka yao mahakamani.

Baada ya kuagizwa kulipa dola bilion 1.527 kama gharama za matunzo ya mtoto na malipo ya wakili katika kesi ya gharama za matumizi na malezi (child support) ya familia yake iliyokuwa ikimkabali.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post