Tyga na Avril waanza upya

Tyga na Avril waanza upya

Ebane! Huko majuu kumenoga hatari famasiala na mapenzi wewe, bwana baada ya kusitisha uhusiano wao wiki chache zilizopita, wasanii kutoka Marekani Avril Lavigne na Tyga waungana tena kama wapenzi.

Imeelezwa wawili hao wamerudiana baada ya kutengana na walionekana pamoja kwenye sherehe ya Sikukuu ya Uhuru nchini Marekani Julai 4 huko Nobu, California.

Ingawa wapenzi hao walikuwa bado wakikutana na kuzungumza baada ya kuachana kwao na huwenda kuimarika kwa mawasiliano baina yao inaweza kuwa chanzo cha kurejesha upendo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags