Twiga amuua mtoto, Afrika kusini

Twiga amuua mtoto, Afrika kusini

Oooooh! Watu wangu wa nguvu natumai ni wazima wa afya basi bwana kila siku kunatokea mambo mazito katika hii dunia, kubwa kuliko ni kuhusiana na Twiga kumuua mtoto mchanga wa miezi 16 katika mbuga ya wanyama huko Afrika Kusini.

Mtoto huyo na mama yake mwenye umri wa miaka 25 walikuwa katika mbuga hiyo kaskazini mwa KwaZulu-Natal wakati wote wawili walipokanyagwa na twiga.

Mtoto huyo alifariki baada ya kupelekwa katika zahanati iliyoko karibu kwa ajili ya matibabu, huku mama wa mtoto huyo alipelekwa hospitalini, akiwa katika hali mbaya, msemaji wa polisi aliviambia vyombo vya habari vya eneo hilo.

Kama mtunavyojua ni nadra mno kwa twiga kuwashambulia wanadamu, hata hivyo uchunguzi unaendelea.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags