Twalhat Kione, Graphic Desginer anayeamini kwenye kujaribu

Twalhat Kione, Graphic Desginer anayeamini kwenye kujaribu

 

Na Aisha Lungato

Mambo vipi! Natumai uko powa mtu wangu wa nguvu, ni jumanne na siku kama ya leo tunakuletea makala kuhusu biashara kwa vijana walio vyuoni.

Tunawaangazia wanavyuo waliopo chuoni kwa sababu tunaelewa kuwa wamekuwa wakijishughulisha na biashara mbalimbali kwa lengo ya kujipatia kipato.

Hata hivyo tumekuwa tukiwaona wadada wengi wanajishihurisha na biashara nyepesi nyepesi kama vile saloon, kuuza nguo nk lakini leo bwana nimekuletea binti flani hivi ni mdogo kimwonekano lakini mambo yake anayo yafanya ni balaa waswahili wenyewe wanakwambia hatari na nusu.

Kila binadamu hufanya biashara anayoipenda na kuikubali na wengi wetu hufanya biashara kwa kupitia vipaji vyao, kufanya graphic and designer limezoeleka ni kazi ambayo hufanywa na watoto wa kiume tu. Leo nakuletea binti ambae anajishuhurisha na biashara ya graphics and designe.

Huyu si mwingine ni Twalhat Kione ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili kozi ya Bachelor in Art and designer ambae anajishuhurisha na biashara ya graphics designer.

Biashara hiyo inamsaidia kutatua matatizo yake madogomadogo kama vile kulipa kodi ya pango, kujinunulia mavazi na chakula.

Kwanini uliamua kufanya biashara hiyo na siyo nyingine

Niliamua kufanya biashara hiyo kwanz katika kozi ambayo ninasoma kuna somo la graphic and designe so nikaona kama opportunities kwa sababu watu wengi ni waoga wa kujaribu especially wanawake.

 

“Nikaona kama wanawake wanaofanya graphics designe ni wachache harafu am talented and am creative that why nikaamua kufanya hii biashara” amesema

Anaongeza kwa kusema “Kwenye kila biashara lazima kuwe na changamoto haijalishi ni kubwa ama ndogo lakini changamoto ni changamoto tu kwa upande wa mwanadada huyu alifunguka na kusema changamoto zake yeye anazokumbana nazo,” anasema.

Hata hivyo anaendelea kusema kuwa changamoto nyingine anayokumbana nayo ni kwenye malipo kwani wapo watu baadhi uingia nao makubaliano lakini ikifika kwenye masuala ya malipo uwa watata.

“Changamoto ipo kwenye payment unakuta unafanya kazi na mtu na kazi ushampatia harafu payment anakuzungusha hii inarudisha vitu nyuma sana, lakini pia hakuna stable payment,” anasema

Pia anasema amekuwa akipoteza baadhi ya wateja kutokana na kushindwa kumuamini kwamba anaweza kufanya kazi kwakuwa tu imezoeleka kwamba zinaweza kufanywa na mwanaume.

So unakuta mtu anakuuliza wewe ni mdada unafanya hii kazi yani anaogopa kabisa kukupatiakazi kwa kuamini kwamba huwezi kumtolea kitu kizuri jambo ambalo si kweli, jamii inapaswa kubadirika katika hili,” anasema

Moja ya kipengele ambacho wafanyabiashar wengi wanakipenda ni suala la faida, kwa upande wa Twalhat ametuambia faida anayoipata kupitia baishara hiyo na amekuwa akiifanyia nini.

Faida ninapata na ninamshukuru Mungu, kupitia biashara yangu hiyo imeniwezesha kununua ovena yangu kwa ajili ya kupika keki so when nikipata muda kila ijumaa napika zangu keki na kuuza” amesema

Kwa vijana ambao wametangulia katika biashara na wakapata mafanikio kidogo lazima watakuwa na mawili matatu ya kuwashawishi vijana wenzao waweze nao kuinuka kwa mwanadada Twalhat ushauri wake kwa vijana wenzake ni

Ushauri ambao nawapa vijana wasiogope kujaribu kwasababu huu ndo umri wa kuhaso huu ndo muda wa kuhangaika hakuna muda mwengine, kwahiyo ukipata nafasi wewe itumie tu vizuri, hangaika, pambana muda utafika wa wewe kula mema bidii zako.

 

Changamoto hazikosekani cha muhimu ni kuweka bidii kwa kila jambo lako pia vijana tusiogope kujaribu kufanya jambo kwa kuhofia kuchekwa kuzarauliwa wewe fanya kitu ambacho moyo wako unakusukuma kufanya hicho kitu” amesema

Katika maisha hata kama uwe na biashara ambayo inakuingizia kipato kila siku, lazima uwe nakitu nje ya hucho ambacho unakipenda zaidi mfano wengine nje ya masomo na biashara upendelea kuingiza, kuimba, kudance na wengine kuogele.

Lakini kwa binti Kione yeye hupendelea zaidi kuchora (Art) na kupaka rangi hivyo muda wake wa ziada huutumia kufanya hayo mabo hivyo basi anawasihi vijana kuwa na muda wa zada.

Vijana wengi wakileo wanaishi kwa kupita njia ya mtu fulani nikimaanisha vijana wengi wa sasa wanandelea sana kuwa kama mtu flani wenyewe wanitaga “role model” kwa mrembo Kione  yeye amefunguka kwa kueleza anatamani kuwa kama nani?

 

Mimi natamani kuwa kama Flaviana Matata kwasababu napenda sana anachokifanya kwa kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji pia anainsper watu wengine mimi napenda sana kuwa kama yeye yani kwangu naweza kusema yeye ndo role model wangu”amesema

Haya haya mdau na mfwatiliaji wa @mwananchischoop funguka hapo chini wewe unatamani kiwa kama nani eeeeh umejifunza nini kutoka kwa mwanadada Twalhati, utanatamani kufanya biashara gani lakini mazingira hayakuruhusu kwa namna moja ama nyingine.

Usiache kufuatilia magazine ya @mwananchisoop ili uweze kujifunza mbinu mbalimbali za kujifunza katika biashara.






Comments 4


  • Awesome Image
    Yusufu

    nami pia napenda graphics ila nafanya kwa kuazima laptop ya mtu

  • Awesome Image
    Yusufu

    nami pia napenda graphics ila nafanya kwa kuazima laptop ya mtu

  • Awesome Image
    Judith

    Congratulations sis❤️ All the best dear Classmate😊✅

  • Awesome Image
    Judith

    Congratulations sis❤️ All the best dear Classmate😊✅

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags