Tumia njia hizi kusave bando Youtube

Tumia njia hizi kusave bando Youtube

Hellow mambo vipi?!! Tupo kwenye kipengele chetu cha kibabe bhana jumatano lazima tuamshe na Smartphone ili kuhakiksha simu zetu tunakwenda nazo sawa bin sawia hakuna kuremba hadi kieleweke ama nini mwanangu mwenyewe.

Ndani ya Smartphone leo nakupa zile tips zitakazo kusaidia kuzuia bando lako kuisha wakati ukiwa umejiachia unachek mavideo kupitia youtube kwenye simu yako.

Kama unavyojua mtu wangu Youtube ndiyo mtandao ambao wengi wetu tunaponea bhnaa tunachek mambo mbalimbali ya kuburudisha kuelimisha lakini sasa mziki unakuja kwenye bandoooo au unasemaje?

Bando linaliwa vibaya mnoo hivyo leo nimeamua kuja kukupa njia ambazo ukizutumia zinaweza kukusaidia kupunguza matumizi makubwa ya data pale unapoangalia video youtube twende sawa sasa.

  • Tuanzie kwenye tips hizi
  • Hakikisha umefungua app ya Youtube kisha bofya kwenye picha yako ya profile ambayo huwa upande wa kulia juu.
  • Baada ya kubofya hapo moja kwa moja bofya upande wa settings ambao unapatikana chini sehemu ya pili kutoka mwisho.
  • Kisha fungua ukurasa mwingine bofya sehemu ya video quality preferences amabayo inapatikana juu, option ya tatu kutoka juu.
  • Enhee baada ya kubofya sehemu hiyo utaona sehemu ya kubadilisha quality za video yaani sehemu ya Wifi na Mobile network, sehemu hii itakusaidia kupunguza quality ya video pale unapoangalia kwenye simu ili isichukue bando zaidi.

Sasa basi ilikufanikisha app ya Youtube isichukue bando zaidi unapotazama video chagua sehemu ya data server, na  hakikisha sehemu hii ya kwanza ya video quality on mobile ndio inakuwa kwenye data server, sehemu hii itasaidia  wakati unaangalia video, data haitatumika kwa wingi kwenye simu yako na hivyo utaweza kuangalia video kwa haraka lakini haitotumia data kwa wingi.

kwenye njia ya kwanza kila video itakubidi kurudi kwenye data server lakini njia ya pili itakua kila ukiangalia video inakua imejiseti yenyewe kazi kwako ipi rahisi kati ya hizo nakuachia wewe.

Njia ya pili unaweza kutumia hii hapa, Ingia kwenye setting > video quality preferences > mobile network > data server.

Ukitumia njia hizi mtu wangu lazima utatoboa tu lakini angalizo ni muhimu sana hapo chini nimekuwekea hivyo kuwa makini sana.

Angalizo:

Ni vyema kukumbuka kuwa sehemu hii hupunguza quality ya video hivyo kama unahitaji kuona video ikiwa angavu sana unaweza kuzima sehemu hii na kuchagua sehemu ya "Auto" au Higher picture quality ambayo huchukua data zaidi.

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags