Tuition binafsi rukhsa, RC Mtaka

Tuition binafsi rukhsa, RC Mtaka

Mkuu wa Mkoa wa Njombe ametoa rukhsa kwa Walimu kufundisha Wanafunzi katika muda wao wa ziada ili kupandisha viwango vya taaluma katika Mkoa huo pamoja na kukuza vipato vyao.

Aidha Mtaka ametoa rukhsa hiyo katika kikao cha uzinduzi wa vitabu vya mwongozo wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa bila kuvunja sheria huku akidai kuwa haoni haja ya kuwazuia kuwa na Tuition binafsi Walimu wakati Kada nyingine wakiwemo Madaktari wamekuwa wakiongeza vipato vyao kwa kuwa na maduka ya dawa.

“Walimu wa Njombe unapomaliza muda wa Serikali nenda kwenye ratiba yako binafsi ili tugawane namna ya kuwaondolea Watoto ujinga kwenye vichwa vyao, fundisheni Mimi nimewapa rukhsa, wakiwauliza waambieni RC ametoa rukhsa sio Afisa Elimu” amesema RC Mtaka

RC amesema hataki kuona Mwalimu akifa Masikini kwakuwa Madaktari wamekuwa na maduka ya dawa, zahanati na wanatibu zaidi ya Hospitali mbili hivyo haoni haja ya kuwazuia walimu kuwa na Tuition ili kujiongezea vipato vyao.

Ooooooooh! Vipi unaungana na RC alicho kizungumza au laaaah dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu.


Comments 1


  • Awesome Image
    George

    Bonafsi naona yukosahihi coz kumnyima mwalimu asiwe na tuition Huku unambana kufanya remedial bila malipo ni uonevu. Chamsingi inatakiwa kuwaambia Tu wasimamie scheme of work ya somo husika kwa vipindi vilivyoko katika utaratibu wa shule na inapofika jioni na siku za weekend waendelee kuwanoa wanafunzi kwa malipo yaziada ya mchango wa wazazi. Elimu ni gharama na mwalimu anamajukumu mengine yakifamilia.

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post