Tuchel agoma kushawishiwa na mashabiki kubaki Bayern Munich

Tuchel agoma kushawishiwa na mashabiki kubaki Bayern Munich

Imeripotiwa kuwa kocha wa #BayernMunich, Thomas Tuchel amedai kuwa hatakubali kushawishiwa na ombi la mashabiki kumtaka abakie katika klabu hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sky Sport News imeeleza kuwa mashabiki zaidi ya 12,000 wamemtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 kusalia katika timu hiyo.

Februari mwaka huu Bayern ilitangaza Tuchel ataondoka katika kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu ambapo ni mwaka moja kabla ya mkataba wake kutamatika.

Hata hivyo kocha huyo ambaye ni raia wa Ujerumani ameweza kuisaidia klabu hiyo kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) na kuchukua taji la Bundersliga msimu uliyopita.

Ikumbukwe kuwa Tuchel aliingia klabuni hapo mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo mkataba wake unamalizika Juni 30, 2025.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags