Trump atumia picha ya Taylor kuomba kura

Trump atumia picha ya Taylor kuomba kura

Mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani Donald Trump ameripotiwa kutumia picha ya Taylor Swift iliyotengenezwa na akili bandia kuhimiza watu kumuunga mkono katika uchaguzi ujao utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Truth Social, mgombea wa chama cha Republican, Trump alichapisha picha ya Swift akiwa amevalia mavazi ya bendera ya nchi hiyo huku picha hiyo ikiwa na ujumbe “Taylor Swift anataka umpigie kura Donald Trump”.

Kufuatia na picha hizo wadau mbalimbali wamejitokeza katika mitandao ya kijamii na kumtaka Taylor Swift amshitaki Trump kwa kutumia picha yake katika kampeni zake bila idhini yake.


Hata hivyo mpaka kufikia sasa Taylor Swift hajatoa tamko lolote kwa umma kama anamuunga mkono mgombea huyo ingawa hapo awali alionesha kuunga mkono wagombea wa chama cha Democratic.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2020 mwimbaji huyo alimuunga mkono Rais ambaye anamaliza madaraka Joe Biden.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags