Trump akutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono

Trump akutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono

Jopo la majaji katika kesi ya madai likuta Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na hatia ya kumnyanyasa kingono mwandishi wa jarida katika duka moja kuu la New York miaka ya 1990.

Ni mara ya kwanza kwa Trump kupatikana na hatia ya kuhusika na unyanyasaji wa kingono. Lakini hakupatikana na hatia ya kumbaka E Jean Carroll katika chumba cha kubadilishia nguo cha Bergdorf Goodman.

Mahakama hiyo pia ilimpata Trump na hatia ya kuharibia jina kwa kuyaita madai ya mwandishi huyo ni uvumi na uwongo na kumuamuru alipe takriban dola million tano kama fidia.

"Leo ulimwengu hatimaye unajua ukweli na ushindi huu sio kwangu tu bali kwa kila mwanamke ambaye ameteseka kwa sababu hakuaminiwa” aliandika Jean Carroll

Aidha wakili wa Trump alisema rais huyo wa zamani anapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags