Trump adaiwa kuagiza chakula akiwa mahakamani

Trump adaiwa kuagiza chakula akiwa mahakamani

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump anadaiwa kuagiza chakula cha haraka maarufu kama MCDonald’s wakati wa kesi yake ya ulaghai wa dola 250 milioni, ikisikilizwa, katika Mahakama ya juu ya Manhattan. 

Baadhi ya watu waliyokuwa nje ya mahakama  walieleza kuwa huenda Rais huyo wa zamani ndiye aliagiza chakula hicho kwani hupendelea kutumia vyakula hivyo, na huonekana sehemu kadhaa akili chakula cha KFC na MCDonald’s.

Kesi hiyo imedumu kwa mwaka sasa baada ya Trump kushitakiwa na Mwanasheria Mkuu wa NY Letitia James ambaye anadai kuwa DT inashutumiwa kwa uongo na ulaghai kwenye ufanyaji biashara.

Hata hivyo inadaiwa kuwa kutokana na kesi hiyo Trump ana uwezekano wa kupigwa marufuku kufanya biashara tena.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags