Msanii Diamond Platnumz anaripotiwa kununua gari zingine mbili aina ya mercedes Benz nyeusi ambapo inaelezwa kuwa moja kati ya hizo haipitishi risasi yaani 'Bullet Proff'.
Taarifa hiyo imewekwa wazi kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa WCB Wasafi baada ya kuchapisha video ikionesha gari hizo huku wakisisitiza kuwa moja ya gari hizo haipitishi risasi.
Diamond anaendelea kuwa kinara kwa wasanii wa Afrika mashariki wanaomiliki magari ya kifahari na gharama zaidi, yakiwemo Rolls- Royce Cullinan 2021, Cadillac Escalade nyeusi, Cadillac Escalade Sky Captain Edition, Toyota Landcruise V8, BMW X6, Toyota Landcruiser TX, Toyota Landcruiser V8 Nyeupe N.k
Leave a Reply