Kesi inayowahusisha ndugu wawili Lyle (56) na Erik Menendez (53), inatarajiwa kusikilizwa tena mahakamani baada ya kugundulika kuwa ndugu hao huwenda wakawa hawana hatia.
Ikumbukwe kuwa mwaka 1989 Lyle na Erik Menendez walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kuwaua wazazi wao Jose na Kitty Menendez kwa kutumia bunduki katika jumba lao la kifahari huko Beverly Hills.
Kesi hio inatarajiwa kurudishwa tena mahakamani ikiwa ni miezi michache tangu filamu ya ‘Monsters’ inayooneshwa katika mtandao wa Netflix kueleza ukweli kuhusiana na kesi hiyo ambapo ndugu wa karibu wa Menendez Brothers waliomba vijana hao kuachiwa huru.
Kupitia tovuti ya BBC kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa tena kwa mara nyingine Januari 30-31 lakini shauri hilo lilisogezwa mbele kufuatiwa janga la moto liliokumba nchi ya Marekani huku ikipangwa kusikilizwa Machi 20-21.
Lyle na Erik Menendez walifikia uamuzi wa kuwaua wazazi wao baada ya baba yao mzazi Jose Menendez kuwafanyia watoto wake unyanyasaji wa kijinsia tangu walipokuwa na umri wa miaka sita, licha ya kumshirikisha mama yao Kitty Menendez, lakini hakuna lililofanyika ndipo watoto hao wakaamua kuwaua wazazi hao.
Hata hivyo wakati wanahukumiwa kifungo cha maisha wakili wa serikali alidai kuwa watoto hao hawakuwahi kufanyiwa unyanyasaji wowote wa kingono bali walitekeleza mauaji hayo kwa sababu ya tamaa za mali kwani wazazi wao waliwaondoa kwenye urithi.
Filamu ya ‘The Menendez Brothers’ iliachiliwa rasmi Oktoba 7, 2024 ikielezea nyuma ya pazia katika kesi ya ndugu hao wawili huku ikiambatanisha na mahojiano ya Lyle na Erik Menendez iliyoongozwa na Alejandro Hartmann
Leave a Reply