Trump adai anaundiwa mashtaka ili kumzuia asigombee urais 2024

Trump adai anaundiwa mashtaka ili kumzuia asigombee urais 2024

Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump adai anaundiwa mashtaka ili kumzuia asigombee urais 2024.

Kauli iliyotolewa na Trump ya kutaka kugombea urais mwaka 2024, inafuatia uamuzi wa Baraza la Wawakilishi linalochunguza vurugu zilizotokea kwenye majengo ya Capitol Hill kuwataka waendesha mashtaka wa Serikali kumfungulia kesi yenye makosa 4.

Mashtaka yanayomkabili Trump ni pamoja na kuzuia shughuli za Bunge la Congress, kula njama za ulaghai dhidi ya Serikali, kutoa taarifa za uongo na kusaidia au kuchochea ghasia.

Aidha Januari 6, 2021, Trump alitoa hotuba kali nje ya Ikulu akidai alishindwa uchaguzi kwa kuibiwa kura na timu ya Rais Joe Biden, kitendo kilichozua hasira za maelfu ya wafuasi wake waliovamia Capitol Hill na kuwashambulia polisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags