Tiwa Savage aweka wazi kutumiwa mkanda wa Ngono

Tiwa Savage aweka wazi kutumiwa mkanda wa Ngono

Niajee leo kwenye gumzo mitandaoni waswahili wanasema mambo si mambo bwana, Staa wa muziki nchini Nigeria Tiwatope Savage maarufu kama Tiwa Savage ametumiwa mkanda wa ngono(sex tape) unaye muonesha yeye na kijana aliekuwa naye kwenye mahusiano kwasasa.

Tiwa Savage amefunguka hayo akiwa katika mahojiano na chombo cha habari nchini Marekani kinacho fahamika kwa jina la “The angle martin show”(power 105.1).

“Jana nikiwa njiani kwenye gari yangu meneja wangu alinitumia ujumbe (massege) kwamba kuna video ametumiwa niitazame, Niloshtuka pindi nilipoiona na kujiuliza ameitoa wapi ilikuwa ni kama baada ya dakika 20 tuu tangu niondoka kwa mtu nilieakuwa na mahusiano naye”amesema Tiwa

Aliendelea kwa kusema kuwa “Nilichanganyikiwa na kumuuliza meneja wangu kuwa tunafanyaje, Meneja akanieleza kiasi anacho kihitaji tumpatie , nikamwambia hapana tukimpatia pesa leo atarudi tena ili kutaka pesa hivyo siruhusu mtu aniibie kirahisi kwa kitu ambacho si halali” amesema Tiwa

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags