Timu ya Lakers yatoa heshima kwa Kobe na mwanaye

Timu ya Lakers yatoa heshima kwa Kobe na mwanaye

Timu ya mpira wa kikapu kutoka Marekani ‘Los Angeles Lakers’ siku ya Jana Agosti 2, imezindua sanamu la marehemu nguli wa kikapu Kobe Bryant na mwanaye.

Kufuatia na taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ‘timu’ hiyo iliweka wazi kuwa lengo la kuzindua sanamu hilo ambalo lilikuwa na mchezaji huyo na binti yake Gianna kama sehemu ya ukumbusho na heshima kwa marehemu hao.

“Heshima hiyo inawakilisha urithi wa kipekee wa mpira wa kikapu kwa Kobe na Gianna na uhusiano mzuri ambao Kobe alishiriki na binti zake wote wanne, katika mchezo wa kikapu” taarifa kwa vyombo vya habari imeeleza.

Utakumbuka kuwa picha iliyotumika kutengenezea sanamu hilo Kobe na Bintiye Gianna waliipiga kwenye mchezo wa Lakers Desemba 2019, huku sanamu hilo likitajwa kuwa la pili kati ya tatu zinazompa heshima mkali huyo wa NBA.

Kobe Bryant na Gianna walifariki kwa ajali ya helikopta iliyotokea Januari mwaka 2020, walifariki katika ajali hiyo Kusini mwa California walipokuwa wakielekea kwenye akasemiki ya Kobe iitwayo ‘Mamba Sports Academy’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags