Timothy mtoto wa Rais wa Liberia aipatia goli marekani kombe la dunia 2022

Timothy mtoto wa Rais wa Liberia aipatia goli marekani kombe la dunia 2022

Timothy Weah, mtoto wa Rais wa Liberia George Weah, aliifungia goli Marekani katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia dhidi ya Wales uliomalizika kwa sare ya bao moja.

Timothy Weah mwenye miaka 22 ni mtoto wa tatu wa Rais wa Liberia George Weah na mama yake Clar raia wa Jamaica, Timothy ni raia wa Marekani kwa kuzaliwa pia ni raia wa Ufaransa na Liberia.

Alifundishwa kucheza soka na baba yake wakati wakiishi huko Marekani, na akiwa na miaka 13 alifanya jaribio la kilujiunga na Chelsea.

Lakini mwaka 2014 alihamia Ufaransa akijifunza soka katika kituo cha PSG na mnamo Mwaka 2018 alitangazwa kuwa katika kikosi cha kwanza PSG timu ambayo baba yake aliichezea miaka ya 90.

Hii si mara ya kwanza kuiwakilisha Marekani kwani alishacheza kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 20 huko India mwaka 2017 na pia aliichezea marekani katika michuano hiyo hiyo ilipo fanyika Poland mwaka 2019.

Tofauti na soka Timothy ni mtayarishaji wa miziki na nikitu anachopenda fanya katika muda wake wa ziada. Hivi sasa Rais George Weah yuko Qatar kwa siku tisa kutazama mwanawe mzaliwa wa Marekani akicheza Kombe la Dunia 2022.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags