TikTok yapigwa marufuku Uingereza

TikTok yapigwa marufuku Uingereza

Mawaziri kutoka nchini Uingereza wamezuia kutimia mtandao wa TikTok katika vifaa vya ofisi. Uamuzi huo umetajwa kuwa ni kwa sababu za kiusalama.

Serikali nchini humo imekuwa ikiamini kuwa mtandao huo unavujisha taarifa muhimu za wateja kwenda kwa Serikali ya China, hoja ambayo imekanushwa vikali na TikTok inayodai ni propaganda za kisiasa.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amekuwa katika shinikizo kubwa kutoka kwa wanasiasa wakongwe wakimtaka afanye zuio kuwa la kiofisi rasmi kama walivyofanya Marekani na Umoja wa Ulaya.

Idara mbalimbali za Serikali na mawaziri wamekuwa wakitumia mtandao wa TikTok wenye watumiaji Bilioni 3.5 kuwafikia vijana na jamii wanayoitumikia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags