The Weeknd Asambaza Mabango Yaliyoandikwa Mwisho Upo Karibu

The Weeknd Asambaza Mabango Yaliyoandikwa Mwisho Upo Karibu

Mwanamuziki kutoka nchini Canada ambaye makazi yake ni Marekani The Weeknd ameingia kwenye vichwa vya habari mbalimbali baada ya kuripotiwa kulipia mabango katika nchi mbalimbali yakisomeka ‘Mwisho upo Karibu’.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini humo zinaeleza kuwa mabango hayo yenye ujumbe huo ambao umewashitua mashabiki wengi yameonekana katika miji kama New York, Miami, Los Angeles, Atlanta na sehemu nyinginezo.

Aidha kufuatia na mabango hayo baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiamini kuwa ujumbe huo ni maandalizi ya Ziara ya kipekee anayotarajia kuifanya msanii huyo mwakani.



Hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kutoa misemo ya aina hiyo kwani mwaka 2021 alitamba na msemo usemao ‘Dawn is coming’ ikiwa na maana ya Alfajiri Inakaribia huku akiitumia kaulimbiu hiyo kama jina la wimbo kutoka kwenye album ya Dawn FM.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags