TBT: UNAIKUMBUKA CHIBONGE YA MARIOO

TBT: UNAIKUMBUKA CHIBONGE YA MARIOO

Leo katika Throw Back Thursday (TBT), tunamkali wa muziki hapa bongo ambaye mwaka 2020 alipata shutuma za kutaka kujinyonga kisa mapenzi, huyu si mwingine ni Omary Mwanga maarufu kama Marioo (Toto Bad).

Mjuba alianza kufanya kazi ya uchomeleaji vyuma chakavu kitaani huku akiwaandikia nyimbo mastaa wakubwa hapa Tanzania kama ile ya ‘Wasikudanganye’ ya Nandy.

Ngoma yake ya kwanza Marioo ilijulikana kwa jina la Dar kugumu ambayo wala haikufanya poa kwenye chats za Bongo hivyo ilimbidi akomae na kuendela kutafuta bomu jingine avimbe nalo mtaani.

Mwaka 2019 mndengereko huyu alitoa kichupa kikamvimbisha sana mjini akimshirikisha Abbah na Gnako ngoma iliyokwenda kwa jina la Chibonge.

Kwa sasa Marioo anafanya fresh na ngoma yake ya AMOR aliomshirikisha Mwanadada Jovial hata hivyo amejaribu kutufungia vioo kwenye mahusiano yake na mwanadada Mimi Mars ila wanazengo wanasema sio siri tena kwani wawili hao mara nyingi huonekana pamoja.

Me naona kwa leo tuishie hapoo mwanangu wa Mwananchi Scoop dondosha comment yako on who you wanna see next on TBT na uniambie ngoma gani ya Marioo inakukosha au sioo...!

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags