Taylor atangaza tarehe ya kutamatisha ziara yake

Taylor atangaza tarehe ya kutamatisha ziara yake

Ikiwa tayari zimefanyika show 100, katika ziara ya dunia ya mwanamuziki wa Marekani Taylor Swift, ‘Eras Tour’, hatimaye msanii huyo ameweka wazi tarehe ya kutamatika ziara yake.

Taylor akiwa katika tamasha lake jijini Liverpool siku ya jana Alhamis Mei 13, 2024 alifichua kuwa ziara yake itatamatika Desemba 8 mwaka huu.

“Ninakiri kuwa ziara hii itakamilika Desemba, nahisi kama ndiyo tumecheza onesho letu la kwanza kwenye ziara kwa sababu mmenifurahisha sana” amesema

Katika ziara yake hiyo amewahi kutembelewa na nyota kama Blake Lively, Ryan Reynolds, HAIM, Bradley Cooper, Gigi Hadid, Kelce na wengineo.

Eras Tour, iliyohusisha mabara matano na kufikisha maonesho 100, ilianza rasmi Machi 17, 2023 Glendale, Arizona, Marekani ikitarajiwa kutamatika Desemba 8, 2024 Vancouver, Canada.

Ikiwa katika muendelezo wa ziara hiyo April mwaka huu msanii huyo alitajwa kuingia katika orodha ya matajiri duniani akiwa anamiliki utajiri binafsi wastani wa dola 1.1 bilioni ni sawa Sh 2.5 trilioni huku idadi hiyo ya fedha ikimfanya kuwa mtu wa 2,545 kati ya 2,781 ya mabilionea wa mwaka 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags