Tatizo la msongo wa mawazo kwa wanachuo

Tatizo la msongo wa mawazo kwa wanachuo

Na Michael Onesha

Msongo wa mawazo ni hali ya shinikizo la kiakili au kihisia linalotokana na mahitaji yanayofikiriwa. Kila siku tunakabiliwa na hali nyingi ngumu ambazo viumbe wanaweza kuviona kama "vitisho" (kwa mfano, mzigo mkubwa wa kazi na kutunza familia zetu).

Suala la msongo wa mawazo kwa wanafunzi limekuwa jipu kutokana na malimbikizo mengi ya mambo yanayozunguka katika akili za wanafunzi hao. Na kabla hatujaenda mbali tuangalie aina ya mzongo wa mawazo kwa mwanadamu

Aina za msongo wa mawazo
Wanasaikolojia wamegundua aina tatu za msongo wa mawazo,
Msongo mkali - husababishwa na shinikizo na mahitaji ya kila siku ambayo sisi sote tunapitia. Inaelekea kudumu kwa muda mfupi. Wakati mwingine dhiki huhisiwa baada ya ukweli kama dhiki ya kihisia au usumbufu wa kimwili.

Msongo wa vipindi: msongo wa mawazo huu unakuwa ni ule wa kili kipindi kikifika mfano, mwezi wa 6 unadaiwa kodi huu ni msongo wa mawazo ambao kila muda ukikaa utawaza kuwa mwezi fulani nadaiwa hichi au natakiwa kufanya hichi, msongo huu wa mawazo unasababisha ugonjwa wa moyo.
Msongo wa muda mrefu - mvutano wa muda mrefu kutokana na matatizo ya ndani au nje, na kusababisha matatizo ya afya na mfumo wa kinga dhaifu. Haya ni mafadhaiko kama vile majukumu mazito ya malezi au kazi ambayo inaoneshwa mara kwa mara inasababisha kiwewe.

Na hii ni mikakati mitano ya kukabiliana na msongo wa mawazo chuoni
Mfadhaiko ni sehemu ya maisha na wakati mwingine hatuwezi kubadilisha hali, lakini tunaweza kujifunza kutambua kile kinachotusababishia hali hii na kukabiliana na athari zake. Lakini kwa upande wa wanafunzi hususani vyuoni wamekuwa wakijipa mawazo kwa kujitakia kutokana na kutamani maisha ambayo hawawezi kuyafikia.
Ili kuepukana na msongo wa mawazo zingatia haya…..

1. Tambua vichochezi
Tengeneza orodha ya vyanzo vyote vya msongo wa mawazo katika maisha yako ya sasa na vikadirie kati ya 10. Anza kwa kutanguliza mambo yanayopaswa kufanywa kwanza na jiulize kama unaweza kuepuka msongo usio wa lazima kwa kuwagawia watu wengine, kuacha kazi ambazo si za lazima.

Unachotakiwa kukifanya wewe kama mwanafunzi ukiona kuna baadhi ya mambo yanakuchanganya basi unatakiwa kuachana na mengine yote na kuzingatia masomo yako kwanza.

2. Zingatia mtindo wa maisha.
Hakikisha unakula lishe bora, fanya mazoezi mara kwa mara (ili kuondoa homoni za mfadhaiko kupita kiasi na kukusaidia kulala vizuri), na kupata usingizi wa kutosha.

3. Tengeneza ratiba yenye uwiano
Tenga wakati wa shughuli na watu wanaokuletea furaha na raha, jifunze kukataa madai ambayo yanaleta msongo zaidi katika maisha yako.
Ukiwa kama mwanafunzi tena wa chuo kikuu or chochote tayari wewe ni mtu mzima na unamaamuzi ya kusema ndiyo au hapana, ukiona jambo linakupa mawazo basi achana nalo litakusaidia hata ukiwa kazini kukataa mambo ambayo yanaweza kukuumiza hapo baadaye.

4. Jenga tabia ya kufanya mazoezi ya kila siku
Kufanya mazoezi kama vile kupumua kwa kupandisha pumzi na kushusha, utulivu wa misuli, yoga au kutembea kutakusaidia kupunguza mawazo katika akili yako.

5. Badilisha matarajio kuhusu maisha ya baadaye
Wanafunzi wengi haswa wa vyuo vikuu wamekuwa wakiishi katika emagination za maisha ambayo hata wazazi wao hawakuyaishi, ili kupunguza vitu ambavyo havina umuhimu katika akili yako unatakiwa kuacha kufikiria kuishi maisha ya kitajiri kuwa na vitu vizuri kuishi kama mastaa mbalimbali so achana na mawazo haya na uanze kuishi maisha yako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post