Tanzania mambo magumu Olimpiki, yakosa medali nyingine

Tanzania mambo magumu Olimpiki, yakosa medali nyingine

Matumaini ya Tanzania kupata medali katika michezo ya Olimpiki 2024 sasa yamebakia kwa wakimbiaji wanne baada ya leo muogeleaji Sophia Latiff kushindwa kufua dafu katika shindano la kuogelea Mita 50 freestyles

Latiff ameshika nafasi ya mwisho katika Heat 5 akitumia sekunde 28:42 huku kinara akiwa ni Jovana Kuljaca kutoka Montenegro.

Kwa matokeo hayo, Sophia ameshindwa kutinga nusu fainali na hivyo atarejea nyumbani kama ilivyo kwa mwenzake wa kuogelea, Collins Saliboko na mcheza judo, Andrew Mlugu.

Katika Heat 5, Latiff alikuwa anashindana na Kuljaca, Rach Christina (Eritrea), Aphenie Greene (St Vincent & Grenades), Georgia-Leigh Vele (Papua New Guinea), Eliane Douillet (Benin), Khema Elizabeth (Shelisheli) na Kaiya Brown kutoka Samoa.

Waogeleaji 16 wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kufanya vyema katika Heats zao.

Waogeleaji hao ni Sarah Sjoestroem, Katarzyna Wasick, Gretchen Walsh, Shayna Jack, Meg Harris, Yufei Zhang, Michelle Coleman na Wu Qingfeng.

Wengine ni Taylor Ruck, Beryl Gastaldello, Kepp Jensen, Neza Klancar, Sara Curtis, Gaspard Florine, Anna Hopkin na Valerie Van Roon.

Wanamichezo wa Tanzania waliobakia ambao watapeperusha bendera kwenye Olimpiki ni Alphonce Simbu na Gabriel Geay watakaokimbia katika Marathoni kama ilivyo kwa Magdalena Shauri na Jackline Sakilu.

Imeandikwa na Charles Abel






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags