Tamasha la Taylor Swift lapigwa chini

Tamasha la Taylor Swift lapigwa chini

Matamasha matatu ya mwanamuziki Taylor Swift yaliyopangwa kufanyika nchini Austria yamesitishwa kufuatia shambulio la kigaidi lililopangwa kufanyika jijini Vienna.

Tishio hilo la usalama lilipelekea wanaume wawili kukamatwa siku ya jana Jumatano Agosti 7 kwa tuhuma za kupanga kushambulia katika eneo la mji mkuu wa Austria.

Taarifa ya kusitishwa kwa show hiyo iliyotolewa na timu ya Taylor Swift

“Kutokana na uthibitisho wa maafisa wa serikali kuhusu shambulio la kigaidi lililopangwa kufanyika katika uwanja wa Ernst Happel, hatuna la kufanya ila kufuta maonesho matatu yaliyopangwa kwa usalama wa kila mtu."

Tamasha hilo ni mwendelezo wa ziara ya kidunia ya Taylor Swift iitwayo ‘Swift's Eras’ ambapo nchini Austria ilipangwa kufanyika Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi kwenye Uwanja wa ‘Ernst Happel’ huku tamasha hilo likitarajiwa kuhudhuliwa na zaidi ya watu 65,000 ndani ya uwanja na wengine 22,000 nje ya ukumbi huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags