Tamasha la Jay-Z lasitishwa

Tamasha la Jay-Z lasitishwa

Tamasha la Made In America linalofanywa kila mwaka na nyota wa muziki Jay-Z lililotarajiwa kufanyika mwezi ujao Philadelphia limeghairishwa hadi mwaka ujao.

Kughairishwa kwa tamasha hilo kumeonekana kuwaumiza mashabiki waliotegemea kufurahi na Jay Z pamoja na wasanii wengine waliokuwa wametarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Tamasha hilo lilitarajiwa kuanza Septemba 2-3 Philadelphia, lakini hadi sasa bado hazijatajwa sababu maalum za kughairishwa kwake.

Kila mwaka tamasha hilo limekuwa likifanyika tangu mwaka 2012, isipokuwa mwaka 2020 lilishindikana kutokana na janga la COVID-19. Kati ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa kuimba siku hiyo ni Miguel, Tems, Metro Boomin, Ice Spice, Coi Leray, Latto, Lil Yachty, Doechii, Lola, na wengine wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags