Tamasha la Jay-Z lapigwa chini tena

Tamasha la Jay-Z lapigwa chini tena

Tamasha la mwanamuziki Jay-Z liitwalo ‘Made In America Festival’ ambalo hufanyika kila mwaka mwezi Mei jijini Philadelphia nchini Marekani lapigwa chini kwa miaka miwili mfululizo huku sababu za kufanya hivyo bado hazijawekwa wazi.

Taarifa hiyo imewekwa wazi kupitia ukurasa wa Instagram wa tamasha hilo kwa kueleza kuwa waandaaji wamejitahidi kwa uwezo wao lakini ‘Made in America’ haitoweza kufanyika kwa mwaka 2024 huku wakiwaahidi mashabiki kurejea wakiwa ngangali.

‘Made in America Festival’ ni tamasha la muziki la siku mbili, lililoanzishwa na ‘rapa’ Jay-Z mwaka 2012, linalofanyika kila wikiendi ya Sikukuu ya Wafanyakazi kwa lengo la kuwakusanya wadau mbalimbali wa muziki pamoja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags