Tafiti zinasema homa ya Nyani husambaa kabla ya dalili kujitokeza

Tafiti zinasema homa ya Nyani husambaa kabla ya dalili kujitokeza

Tafiti zinaonyesha watu wenye maambukizi ya homa ya nyani wanaweza kuwaambukiza wengine siku nne kabla ya dalili kuanza kijitokeza huku kukiwa na mashaka kwamba zaidi ya nusu ya maambukizi huenda yakatokea katika kipindi hiki hii ikiwa ni kulingana na makadirio ya utafiti huo uliofanyika nchini Uingereza.

Ingawa utafiti huo bado haujathibitishwa lakini unahitimisha kwamba maambukizi mengi ya homa ya nyani hayawezi kuzuilika kwa kuwaomba wagonjwa kujitenga mara wanapoanza kuona dalili.

Utafiti huo mpya uliochapishwa katika jarida la afya la BMJ la nchini Uingereza taifa la kwanza kubaini visa vya maambukizi ya homa ya nyani nje ya Afrika.

Shirika la kimataifa la afya, WHO limesema watu 36 wamekufa na zaidi ya 77,000 wameambukizwa maradhi hayo tangu mwezi Mei wakati virusi vya homa hiyo vilipoanza kusambaa ghafla katika mataifa ya Afrika ya Magharibi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags