Tabia ya kuzoeana inavyoweza kuharibu mahusiano na ndoa yako

Tabia ya kuzoeana inavyoweza kuharibu mahusiano na ndoa yako

Helooow! Natumai ni wazima wa afya sasa bwana leo kwenye mahusiano nimekuja kukomesha kile kitendo ama kauli ya kuwa mmezoeana bila ya kujua itaawathiri vipi nyie wote kwa pamoja.

Kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla.

Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini.

Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinna, nguo za fashion, salon, manukato, kujipamba na dhahabu huyafanya pale anapotoka kwenda harusini na sio nyumbani. Huku ndio kuzoena, na tafsiri sahihi ni kudharau.

Mambo haya yanaweza kukukosti mana wanaume wengi wanapenda wanawake wao wawe wasafi na muonekano mzuri kila siku na kila time, ndo mana unaambiwa ukishaingia kwenye ndoa kila baada ya siku 15 inabidi uwe na muonekano mpya kwa mumeo.

Kama hujui leo nakujuza mambo ya kusema mmezoeana ndo chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika na mahusiano pia kuvunjika, hii ni kauli ambayo itakuja kukukost baadae ambapo utakuwa ushachelewa. Hivyo ili kulinda kibarua cha chako cha mahusiano ni vyema ukajifunza kila wakati kutofanya vitu ambavyo vimekuwa havijayajengi mahusiano yako.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags