Sura ya Rihanna kutumika kwenye manukato ya ‘Dior’

Sura ya Rihanna kutumika kwenye manukato ya ‘Dior’

Mwanamuziki kutoka visiwa vya Barbados, #Rihanna amepata shavu katika kampuni ya ‘Christian Dior’ inayojihusisha na masuala ya utengeneza nguo na urembo kwa kutengeneza perfume zenye sura ya Rihanna ‘Riri’.

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes imeeleza kuwa kampuni hiyo imetangaza kutoa mwonekano wake mpya wa manukano ya ‘Dior J’ Adore’ unaotarajiwa kutoka mwezi Septemba mwaka huu utakuwa na sura ya Rihanna ‘Riri’.

Aidha inaelezwa kuwa katika kampuni hiyo maarufu kupitia bidhaa zake ulimwenguni, kuweka sura ya Rihanna ni makubaliano makubwa kuwahi kutokea kwa takribani miaka 20 iliyopita.

Hata hivyo kwa upande wa mwanamuziki huyo ameeleza kuwa ni heshima kwake sura yake kutumika kwenye ‘Dior J’adore’ kwani ilikuwa ni moja ya ndoto zake kuonekana katika chapa maarufu kama hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa manukato hayo #VéroniqueCourtois naye amesema kuwaa anajivunia sana kumkaribisha Rihanna katika familia ya Dior huku akiamini kuwa kubadili sura ya Rihanna kutaleta matokeo makubwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags