Studio ya Jux kama kwa Diddy

Studio ya Jux kama kwa Diddy

Wanamuziki kutoka nchini Diamond, Jux, Billnass, Mbosso na mtayarishaji S2kizzy (Zombie) wako jikoni kuandaa ngoma ya pamoja ambapo kupitia video inayosambaa mitandaoni inawaonyesha wasanii hao wakiwa katika studio ya Jux.

Aidha katika video hiyo moja ya sauti iliyosikika zaidi ilikuwa ikisema kuwa studio hizo za Jux ni kama kwa mkali wa Hip-hop kutoka nchini Marekani, Diddy akimaanisha kuwa ukiimba vizuri unapewa tuzo za Grammy.

Hii siyo mara ya kwanza kwa wasanii hao kufanya ‘kolabo’ ya pamoja kwani Diamond na Jux wamefanya ngoma iitwayo ‘Enjoy’ ambayo inaendelea kufanya vizuri kupitia mtandao wa YouTube, vilevile Mbosso alishawahi kutoa ngoma na Mondi iitwayo ‘Baikoko’, huku Billnass akiwa bado hajatoa kolabo yoyote lakini wiki iliyoisha walitoa kionjo cha ujio wa ngoma yao mpya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags