Stevie Wonder sasa ni raia wa Ghana

Stevie Wonder sasa ni raia wa Ghana

Mwanamuziki wa Marekani Stevie Wonder sasa ni raia wa Ghana baada ya kula kiapo cha utii na kupokea cheti cha Uraia kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Nana Akufo-Addo jana Mei 13, 2024.

Mkali huyo wa R&B aliyezaliwa Saginaw, Michigan, Marekani, alikula kiapo hicho katika siku yake ya kuzaliwa, jana akiwa anatimiza miaka 74 katika Ikulu ya Jubilee jijini Accra,  Ghana. Hata hivyo atakuwa raia wa nchi zote mbili Marekani na Ghana

Stevie Wonder siyo msanii pekee ambaye amekuwa akiutaka uraia wa Ghana kwani mwanamuziki Meek Mill naye ni mmoja wa wasanii ambao wanaitaji uraia wa nchi hiyo na kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali vinaweka wazi kuwa huenda ‘rapa’ huyo naye akakubaliwa kuwa raia wa Ghana siku chache zijazo.

Baadhi ya kazi zilizomtambulisha Wonder ni pamoja ngoma ya ‘Superstition’, ‘Sir Duke’, ‘I Wish’ na ‘I Just Called Sema I Love You’. Amerekodi zaidi ya vibao kumi bora vya U.S. na kupokea Tuzo ishirini na mbili za Grammy, tuzo ambazo zilimfanya kuwa msanii pekee wa kiume kuwahi kupata tuzo nyingi.

Hata hivyo mwaka 1994 alifanikiwa kutunukiwa nyota ya heshima ya ‘Hollywood Walk of Fame’ ikiwa kama pongezi kutokana na makubwa aliyoyafanya katika tasnia ya muziki nchini Marekani.

Wonder pia anajulikana kwa kazi yake kama mwanaharakati wa masuala ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na kampeni yake ya 1980 ya kufanya siku ya kuzaliwa ya Martin Luther King, Jr kuwa likizo nchini Marekani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags