Baada ya filamu ya Squid Game Msimu wa 2 kufanya vizuri na kupata rekodi za kutosha, hatimaye wasambazaji wa filamu hiyo Netflix wametangaza tarehe rasmi ya kuachia filamu hiyo msimu wa tatu.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia video fupi ya matangazo kupitia chaneli ya YouTube ya Netflix Korea ambayo imeweka wazi kuwa filamu hiyo itaanza kuoneshwa kwa mara ya kwanza 27, Juni 2025.
Kutokana na taarifa hiyo mashabiki na wadau mbalimbali wamefurahishwa na taarifa hiyo huku baadhi yao wakitaka filamu hiyo iendelee kutoka kila mwaka.
Squid Game msimu wa pili iliachiwa rasmi Desemba 26, 2024 huku ikichezwa na mastaa mbalimbali wakiwemo Lee Jung-jae, Lee Byung-hun, Wi Ha-jun, Gong Yoo na wengineo.
Leave a Reply