Sony music wanunua nusu ya kazi za MJ

Sony music wanunua nusu ya kazi za MJ

Kampuni ya muziki kutoka nchini Marekani ‘Sony Music’ imeripotiwa kununua asilimia 50 ya nyimbo za marehemu Mfalme wa Pop Michael Jackson.

Dili hilo limekamilika kwa msaada wa familia ya marehemu MJ ambapo wamefanikiwa kuuza nyimbo alizoziandika na kuzirekodi Mj mwenyewe, kwa dola 1.3 bilioni ambazo ni sawa na tsh 3 trilioni.

Nyimbo ambazo MJ aliziandika mwenyewe ni kama ‘Heal the World’, ‘Earth Song’, ‘The Way You Make Me Feel’, ‘Will You Be There’, ‘Bad’, ‘Childhood’, ‘Wanna Be Starting Something’, ‘I Just Can't Stop Loving You’, na nyinginezo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post