Soma hii kama unajiskia vibaya kwenda diploma wakati rafiki zako wako degree

Soma hii kama unajiskia vibaya kwenda diploma wakati rafiki zako wako degree

Hellow! Naona ni week ya kufungua shule na vyuo vyote ambapo baadhi walikuwa katika likizo fupi ya sikukuu, so tumekusogezea mada hapa ambayo kunabaadhi ya wanafunzi wanajiskia vibaya kuana wenzao wanaenda degree na wao wanabaki kuanza diploma. Sasa soma hii ili uachane na fikra potofu ya kujizarau na kusema kuwa wewe huwezi.

Kwenda diploma wakati watu wote uliosoma nao wanaenda kusoma degree chuoni ni kitu kinachoumiza na kukufanya ujisikie vibaya. Na muda mwingine hao watu unaweza kuwa nao chuo kimoja hivyo mnaonana kila siku weeeh! Asikwambie mtu inauma bwana.

Kwa wale wanaoenda kusoma diploma chuoni, wakati wengine mliokuwa nao wanaenda degree ningependa niwatie moyo kwa mambo haya machache…

  • Kwanza, kila mtu kwenye maisha ana safari yake

Hata kama mlianza wote shuleni, kila mtu kwenye maisha ana safari yake na jinsi mambo yake yatakavyomwendea, Hata mtakaokuwa wote diploma mkimaliza wengine wataendelea, wengine wataenda kazini, na wengine watachukua jukumu la kuolewa Kila mtu anasafari yake, hivyo sasa hivi inabidi ukubali kuwa safari yako ni tofauti na ya wengine, na hivyo ndivyo maisha yalivyo.

  • Pili, maisha siyo mashindano

Kwenda diploma sio kwamba umeshindwa, na wao kwenda degree sio kwamba wameshinda maisha sio mashindano maisha ni safari kama tulivyo sema hapo mwanzo na kama ni safari kila mtu atapanda usafiri wake.

Kila mtu anatembea peke yake kwenye hiyo safari, hakuna mtu anayeshindana na mwengine kwenye hiyo safari, hivyo usijisikie kama umeshindwa kwenye safari ya maisha yako, muda mwingine hivyo ndivyo safari yako ya maisha ilivyopangwa kuwa. 

  • Tatu, hauwezi jua kusudi la wewe kwenda diploma

Huwezi jua unapoenda diploma Mungu amekupangia nini huko, hauwezi jua njia hii unayopitia ina nini kwaajili yako na maisha yako ya baadae, labda diploma utakuja kupenda kusomea jambo jingine kwaajili ya degree? Hakuna ajuaye kesho yake.

  • Nne na mwisho kabisa muda mwingine mipango yetu, mambo tunayoyataka hayatokei kama tunavyotaka yawe ila maisha inabidi yaendelee

Kuliko kukaa na kujidharau, kujihuzunikia, muda mwingine ni jambo zuri kukubali kuwa sisi tunapanga, Mungu anacheka. Mipango tunayopanga muda mwingine haiendi kama tunavyotaka iende na hivyo hatuwezi kuilazimisha, mambo mengine yako nje ya uwezo wetu wa kuyafanya yatokee kwa wakati tuutakao.

Sio jambo baya kusoma diploma, sio jambo la kudharaulika au kudharauliwa au kujidharau. Ni jambo la heshima kusoma, level yoyote ile unayosoma. I’m so proud of you kwa kwenda kusoma. Jikubali safari moja ndogo huanzisha safari nyingine kubwa zaidi

Natumai utapona na kujisikia vizuri kwa level hii uliyopata kusoma kiasi kwamba maneno ya mtu au watu wanavyokufikiria haikuumizi. Ila inakutia moyo kuendelea maana safari yako ya maisha ni tofauti na yao.

Cha muhimu cha kukizingatia na kukijua ni kuwa “Rizki” ukishaelewa hili neno basi mambo yote utayaona yakawaida sana kwasababu kila mwanadamu na rizki yake ambayo mwenyezimungu atamjaalia na atampitisha. Acha wakati wa mungu utende miujiza






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post