Snoop Dogg kuacha kuvuta sigara ilikuwa ni kiki

Snoop Dogg kuacha kuvuta sigara ilikuwa ni kiki

Ni siku tano tuu zipite tangu ‘rapa’ kutoka nchini Marekani Snoop Dogg kutangaza kuacha kuvuta sigara, hatimaye imegundulika kuwa ilikuwa ni kiki ya tangazo la kampuni ya majiko.

#Snoop kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share video akiwa anatangaza jiko hilo la ‘Solo stove’ huku akidai kuwa hajaacha kuvuta sigara bali ameacha kutumia majiko yanayotoa moshi.

‘Solo stove’ ni aina ya majiko ambayo yanatoa moto bila ya kutoa moshi.

#SnopDogg anatamba na ngoma zake kama vile ‘Doggyland’, ‘Drop It Like It's Hot’, ‘Lay Low’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags