Siri za kufanya biashara ya nguo mtandaoni

Siri za kufanya biashara ya nguo mtandaoni

Niajeeee!!! Mwanangu mwenyewe je unajua siri za kufanya biashara yako ya nguo ifanikiwe mtandaoni? Mambo yasiwe mengi bhana ni vitu vidogo sana leo kwenye Nipe Dili nakukunjulia mchakato mzima.

Ni rahisi tu wala usichanganyikiwe inawezekana kabisaaa!! Nawe kula kuku kwa mrija ukifurahia jitahada za biashara yako, wauzaji wengi wanaofanikiwa katika biashara ya nguo mtandaoni ni wale ambao nguo zao zinaendana na wakati.

Lakini si hivyo tu kuna hili nalo nguo ambazo haziuzwi na kila muuzaji ushanifahamu hapo? Hapa nakuletea Siri nne aadhwimu zitazokuwezesha kuwa mfanyabiashara wa nguo mwenye kufanikiwa kupitia mitandao ya kijamii.

Tumia sanamu kuonyesha muonekano wa nguo unazouza

Hapa bhna ni muhimu sana itakurahisishia watu kuvutiwa na nguo zako kwani mtu akiona nguo imewekwa vizuri kwenye sanamu kishepu kipo aaah wewe lazima avutiwe tu niamini mimi nakwambia.

Unaweza kuanza na mdoli unaoonyesha sehemu tu mwili unavyotaka kuonyesha nguo au kama mtaji wako unaruhusu basi unaweza kununua mdoli anayenyesha nguo zote zinavyokaa mwilini kama unaweza tumia mtu azivae.

Weka jina Rangi na Aina ya Nguo kwenye Tangazo lako

Katika ulimwengu wa teknolojia, mitandao ya kutafutia data kama vile Google imeboreshwa sana kufanya watafutaji kupata vitu kwa urahisi  mfano mtu anataka nguo Fulani akienda google akiandika tu nguo anayoitaka basi tangazo la nguo zako litatokea endapo tu maneno maneno hayo yatakuepo kwenye tangazo lako.

Ni muhimu pia kufahamu wanunuzi wwako wanatumia maneno gani wakati wanatafuta bidhaa kama unayouza wewe.

Hakikisha picha za nguo zinaonekana pande zote

Hili nalo lakuzingatia hakikisha unamsaidia mnunuzi wa nguo kupata picha jinsi atakavyoonekana akivaa hiyo nguo kama ni gauni au T-shirt hakikisha picha unazozipigania zinaonesha pande zote za nguo hiyo mbele, nyuma na pembeni.

Onesha kwa umakini maeneo muhimu ya nguo kama vile Zipu, vifungo vinavyovutia, nembo nk hakikisha tangazo linamfanya mteja akutafute jitahidi picha zijieleze zenyeweee.

Hakikisha unaweka vipimo vya Nguo unazouza

Kwanza ili watu waelewe zaid product yako hakikisha unaweka tangazo lako na vipimo vya nguo, ni muhimu kwa wanunuzi kwa maana itawaonesha kama una nguo za vipimo vyao wengi hawatajisumbua kuchukua namba yako ya simu na kukupigia ili kukuuliza vipimo vyao.

Watakachokifanya watanunua nguo mtandaoni ni kuokoa muda sasa kama muuzaji utashindwa kuwapunguzia wanunuzi wako muda wa kufanya maamuzi basi utawakosa.

Yeeees!!! Sasa kazi ni kwako mtu wangu nimeshakupa maujanja hapo pambania kombe au sio? hard working, respect kuwa Royal kwa wateja lazima utoboeeee nakutakia kazi njema!!!!!!!!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post