Mwanamuziki Barnaba Classic, ameweka wazi siri inayomfanya kuendelea kufanya vizuri kwenye gemu ya muziki akieleza kuwa ni nidhamu, heshima, muda pamoja na ushindani wa vitendo.
“Game inataka nidham, muda, ubunifu, hekima na ushindani wa vitendo sikuzote! kila siku vipaji vinazaliwa wazuri wanakuja na wazamani taratibu wanapisha hizo nafasi eiza kwa makusudi au kwa kutokugundua kama wanapisha bila kujua.
Sasa chamsingi kujua watu wako wanataka kipi Au nini?? Muziki unasema na wale wanaotaka kusemeshwa na hisia kali midundo na tungo zilizo bora kuliko zile za jana au nyakati zilizopita kwa kufanya hivi utabaki bora sikuzote,”ameandika Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram
Aidha ameongezea kwa kueleza “Mopaoontop binafsi nimechagua kuwa mwana mabadiriko sikuzote kwa kusikiliza, kukubali,kupokea na kuheshim nafasi ya kila mmoja ndio mana bado naendelea kuwapa huduma ya miziki mzuri,”
Barnaba amekuwa kwenye gemu ya muziki kwa muda mrefu huku akitoa hitsong nyingi ikiwemo Nabembelezwa, Chausiku, Magubegube, Milele daima, Cheketua, Nibusu na nyinginezo.
Mbali na kujikita zaidi kwenye muziki lakini pia msanii huyo mwaka uliyokwisha alioneakana katika tamthilia maarufu ya ‘Mawio’ akicheza kama Alawi, filamu ambayo ilimuongezea kutambulika zaidi katika tasnia ya burudani.

Leave a Reply