Simi aungana na Wakenya, Aumizwa na waliopoteza maisha

Simi aungana na Wakenya, Aumizwa na waliopoteza maisha

Mwanamuziki maarufu nchini Nigeria, #Simi, ametoa sauti yake katika maandamano ya kupinga ongezeko la kodi yanayoendelea nchini Kenya ambapo amedai kuwa inahuzunisha watu kupoteza maisha kwa ajili ya kupigania uhuru na haki zao.

Simi ameyasema hayo kupitia mtanadao wa X (zamani Twitter)  kwa kuandika ujimbe wa kutoa hamasa na kuunga mkono maandamano hayo huku akisema kuwa kwake ni uhuzuni kuona hali kama hiyo watu wa Kenya kupigania uhuru na haki mpaka kufariki.

“Nasimama na watu wa Kenya ni nguvu na inahuzunisha kwa watu kupigania na kufa kwa ajili ya uhuru na haki” Ameandika

Hata hivyo msanii huyo amesema kuwa hawezi kungoja siku ambayo Afrika itaendeshwa na silaha kutetea nguvu zao na rasilimali huku akidai kuwa hakuna uwezekano wa ustawi mzuri mpaka watu waandamane.

Hiyo ni baada ya watu watano kuripotiwa kufariki siku ya jana Jumanne kwa kupigwa risasi na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati polisi walipo kuwa wanakabiliana na waandamanaji waliovamia jengo la bunge jijini Nairobi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags