Simba wamkaribisha Rais Samia Simba day

Simba wamkaribisha Rais Samia Simba day

Wakati wanajangwani wakitarajia kuachia Documentary yao, wanamsimbazi wao wanajiandaa kusherehekea kilele cha siku ya wanasimba inayotarajiwa kufanyika Agosti 6.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa simba wameweka wazi kuwa mgemi rasmi katika siku hiyo atakuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Simba wame-post picha ya Rais na kuandika,
“Karibu kwenye kilele cha wiki ya Simba, Karibu kwenye simba day, Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Hii ni siku muhimu kwa ‘klabu’ ya Simba na wapenda michezo wote nchini Tanzania.

Tunashukuru na tunakukaribisha kwa furaha kubwa isiyo na kifani. Kwa kipekee kabisa tunashukuru sana kwa mchango wako mkubwa kwenye sekta ya michezo na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, Karibu sana muheshimiwa Rais”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags