Simba na Yanga kukiwasha april 20

Simba na Yanga kukiwasha april 20

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB) imetoa tarehe ya mchezo kati ya ‘klabu’ ya #Yanga na #Simba ambapo ‘mechi’ itachezwa siku ya tarehe 20 mwezi April saa 11 kamili jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa mbio za ubingwa wa ‘ligi’ hiyo unaenda kuchezwa huku ‘timu’ hizo za kariakoo zikiwa zimetoka kuondolewa kwa pamoja kwenye michuano ya ‘ligi’ ya mabingwa Afrika kwenye hatua ya robo fainali.

Ikumbukwe kuwa ‘klabu’ ya #Yanga wanaongoza ‘ligi’ hiyo wakiwa na alama 52 baada ya kucheza michezo 20 huku ‘klabu’ ya #Simba wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na alama 45 baada ya kucheza michezo 19.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags