Simanzi ilivyovamia nyumbani kwa Maria Carey

Simanzi ilivyovamia nyumbani kwa Maria Carey

Mwimbaji wa muziki nchini Marekani Maria Carey (59) amethibitisha kufiwa na mama yake Patricia pamoja na dada yake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika taarifa yake aliyoitoa siku ya Jumatatu Agosti 26,2024 mwimbaji huyo amesema, moyo wake unaumia sana kumpoteza mama na dada yake wikiendi iliyopita.

“Nimempoteza mama lakini chakusikitisha zaidi nimempoteza dada yangu siku hiyohiyo,” amesema

Staa huyo wa R&B raia wa Marekani ameeleza kuwa alijihisi kubarikiwa kwa kutumia muda wake mwingi akiwa na mama yake wiki moja kabla ya kifo chake.

Aidha, Carey mwenye tuzo za grammy 6 hakutoa taarifa yoyote kuhusu chanzo cha vifo vya wapendwa wake hao.

Awali, mwaka 2020 mwimbaji huyo alielezea kwakina uhusiano wake na mama yake wenye visa na mikasa huku akidai mama yake alimsababishia maumivu na mawazo mengi sana wakati wa ukuaji wake.

Patricia,(87) kabla ya kifo chake aliwahi kuwa mwimbaji na kocha wa sauti mwenye asili ya Ireland na Marekani, huku Maria akielezea upendo mwingi aliokuwa nao kwa mama yake na kuandika baadhi ya nyimbo.

Katika mahojiano na Gayle King mnamo 2022 Maria alisema “katika ukuaji wangu mambo yaliyoniathiri sana ni ukosoaji kutoka kwa mama yangu mzazi, lakini pia namshukuru kwa kunitambulisha katika tasnia ya muziki,”alisema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags