Sikukuu bila pilau inawezekana, Pika hivi kufurahisha uwapendao

Sikukuu bila pilau inawezekana, Pika hivi kufurahisha uwapendao

Kama ilivyo kawaida yetu @Mwananchiscoop hatulazi damu, wiki hii katika biashara tunakusogezea mada ambayo haina mambo mengi kabisa kuhusiana na vyakula simple unavyotakiwa kupika siku za sikukuu.

Siku zote huwa tunaongea ukweli, katika pita pita zetu tumegundua kuwa siku za hivi karibuni kwenye nyumba nyingi watu wamekuwa hawafagilii sana kupika tena pilau na ubwabwa (wali) katika siku za sikukuu badala yake wanapika vyakula simple tu na inatokana na vyakula hivyo kuliwa kila siku katika familia zao.

Tumezoea na kujiweka kuwa kila ifikapo sikukuu lazima kupika pilau yaani bila pilau sikukuu hainogi, na litatofautiana kidogo utakuta mara  huyu amepika pilau mbuzi, yule samaki, kuku, nyama firigisi na kama mtu atabadilisha basi atapika biriani.

Mimi leo nitakusogezea menu simple tu itakayokupa muongozo kuelekea katika sikukuu hizi za mwisho wa mwaka kwa familia zinazoanzia watu  watano hadi kumi vipo vyakula ambavyo unaweza kupika na kumfanya kila mtu akaridhika ndani ya nyumba, tuache kujificha katika kivuli cha pilau tujitahidi kubadilisha milo.

Menu simple katika sikukuu za mwisho wa mwaka

  1. Sambusa za nyama, kachori, Eggchop, cake, kuku, nyama ya ngome ya kukaanga au maini rosti.
  2. Tambi, ndizi za kukaanga, donat, mishikaki ya ng’ombe au mbuzi na kuku wa kukaanga.
  3. Chipsi, ndizi nyama (unaweza kuunga kwa nazi au ukapika mchemsho), kuku na unaweza kuongeza na sousage.
  4. Biriani simple si lile lenye mambo mengi, kuku wa kukaanga na rosti la biriani.
  5. Menu nyingine ambayo ni simple sana unaweza kuchinja mbuzi, au kununua kuku na mkungu mmoja wa ndizi, so hapa utawapa option wanaotaka kukaanga watakaanga na wanaotaka kuchoma pia watachoma.

Na katika upande wa vinjwaji, unaweza kutengeneza juice mwenyewe na juice siku hizi zipo nyingi sana utachagua ya embe, tende, tikiti maji au yoyote utakayoona kwako ni sawa, usisahau soda, maji, youghat na matunda aina yote.

Kwa wale wanaopenda kamnyweso pia utawazingatia, na siku hizi kuna vinywaji ambavyo ni Mocktail na Cocktail so kama mfuko wako uko vizuri unaweza tafuta mtu anaejua kutengeneza vinjwaji hivyo akaja nyumbani kwako kukutengenezea.

Licha ya hayo yote kuna zile familia kubwa ambazo watu wakikutana unaweza kusema nyumba ina sherehe ama msiba, siku hizi hakuna kuumiza kichwa mnaweza kujipanga wenyewe na kununua ng’ombe.

Mkachinja na mikungu kadhaa ya ndizi na ukawapa watu nafasi ya kujichagulia kama watakunywa supu, watarosti maini, watakaanga nyama au kuchoma ni wao tu, cha kuzingatia ni vinywaji kuwa vingi, nimesema ng’ombe kwa sababu bei yake haiwezi fika 500k so kwa familia ya watu 20 mnaweza kununua kabisa.

Na kama hamna uwezo wa kufanya yote hayo mnaweza  kupika chakula ambacho kiko ndani ya uwezo wenu nyinyi kama familia, ila katika sikukuu hizi za mwisho wa mwaka hazihitaji mambo mengi.

Ukiachilia mbali familia kujumuika kwa pamoja kuna wale wengine ambao hupendelea kutoka out na kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujivinjari, ushauri wangu kwa sehemu za starehe wajitahidi kupika vyakula simple sana nyama ziwe nyingi, siyo mtu katoka nyumbani kaacha pilau kaja kwenye restaurant yako anakuta wali utamfanya mteja asirudi mara nyingine.

Kwa leo naona tuishie hapa, maana tushaelezana mengi cha kuzingatia nyama ziwe nyingi, vinywaji, kutengeneza kachumbari, pilipili pamoja na matunda ili mambo yote yawe bulbul.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post