Siku moja, sehemu tatu tofauti, watu wale wale

Siku moja, sehemu tatu tofauti, watu wale wale

Kila kitu kimebadilika. Hata Hayati Magufuli naye akiibuka hii leo atastaajabu vitu vingi. Ulitegemea Bunge hili kuwa nje ya mikono ya Job Ndugai?

Ulitegemea Alikiba kuhamia Simba na kuwatungia lile pini tamu? Ama Dimpoz kurudisha ushikaji na Mondi? Atastaajabu sana.

Sasa achana na hizo makitu. Kuna hili la siku moja kuwa na sehemu tatu tofauti. Na kukutana na watu wale wale wanahama tu kwa ajili ya jambo lilelile.

Ilikuwa ni kila siku ya Jumapili. Nyakati zile ana gari kali bila geto, jina kubwa bila kipaji, hela nyingi bila kazi wala ofisi. Hana hata makazi pia.

Kila Jumapili mchana tupo ‘Lidazi Klabu’. Ni mwendo wa Twanga na Kupepeta, pombe nyingi na pisi kali za kutosha. Watoto wa mjini wote watakuwa pale kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja usiku.

Ikifika saa moja usiku robo tatu ya waliojaa ‘Lidazi’, ungewakuta Msasani Klabu. Pale mwendo wa ‘samaki ana vipande vingapi? Hebu vitaje, kichwa, tumbo na mkia.

Wazee wa ‘bling bling’ Fm Academia, hapo ni mwendo wa biere na Ngwasuma mpaka saa sita usiku. Hapo walipiga kuanzia saa moja hadi saa sita usiku.

Wakimaliza, wale wa Lidazi’, ambao robo tatu yao walihamia Msasani Klabu. Hapo napo robo tatu yao, wangeenda TTC Club Chang’ombe, Twanga Pepeta tena.

Twanga walikimaliza ‘Lidazi’, walikusanya vyombo kwenda TTC Chang’ombe. Huko walioingia usiku mpaka usiku wa manane. Nako kulfurika watu.

Mliyekutana ‘Lidazi’ akila bia. Ungemkuta Msasani akila bia zilezile. Chang’ombe nako ungemuona akitafuna bia zake hadi usiku mnenePost Descriptions






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags