Shujaa Majaliwa atinga bungeni

Shujaa Majaliwa atinga bungeni

Majaliwa Jackson, kijana aliyewezesha kuokolewa kwa watu 24 katika ajali ya ndege ya Precision Air katika Ziwa Victoria, iliotokea Novemba 6 mwaka huu, leo amefika Bungeni jijini Dodoma kama mgeni.

Majaliwa ambaye amepokelewa na kuanza mafunzo katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Tanga amekaa katika jukwaa wanapokaa wageni wa Spika wa Bunge.

Nyie nyie, muacheni tuu Mungu aitwe Mungu, ndani ya siku chache, maisha ya kijana mdogo yamebadilika kabisa. Wanangu sana tusikate tamaa, tuendelee kupambana kwa ajili ya kujenga taifa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags