Show ya Nicki Minaj yapigwa kalenda

Show ya Nicki Minaj yapigwa kalenda

Show ya ‘rapa’ Nicki Minaj iliyotakiwa kufanyika jana Machi 18, New Orleans, Marekani ambayo ni muendelezo wa ziara yake imeghairishwa kutokana na mwanamuziki huyo kutokuwa vizuri kiafya.

Katika taarifa iliyotolewa na hospitali ya Smoothie King Center, imeeleza kuwa Nicki hatoweza kufanya show kutokana na changamoto za kiafya, huku maofisa wa ziara ya Nicki wakiwatuliza mashabiki kwa kudai watapanga tarehe mpya ya kufanyika kwa show hiyo.

Ikumbukwe siku mbili nyuma #NickiMinaj alituma ujumbe kupitia mtandao wa X akieleza anahisi kuwa na Corona. Hata hivyo taarifa ya daktari inasema hana ugonjwa huo kama alivyokuwa akihisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags