SHILOLE: Wasanii acheni kudharau watu

SHILOLE: Wasanii acheni kudharau watu

Ebwana moja kati ya story kubwa huko mitandaoni ni hii hapa ambapo mwanadada Mjasiraimali na Msanii pia Shilole ameamua kuwakumbusha wasanii wenzie kuacha dharau kati yao kwa kuamini nafasi walizonazo sasa wanaweza kuwa nazo milele.

Shilole hakuishia hapo aliendelea kusema anawakumbusha kuwa walikuwepo wasanii wengine wakubwa tanzania na walifanya vizuri lakini leo hawapo kwenye charts za muziki.

Aidha Shilole ameyasema hayo alipokuwa akifanyiwa Mahojiano na Waandishi wa Habari

"Kuna Wasanii wengine wanaonaga tayari wamemaliza kumbe hii sanaa bado ni kubwa sana kila mmoja anahitaji kupata mkate wake kwa wakati wake”.

“Kwahiyo tumia wakati wako vizuri lakini kumbuka kuna wasanii wengine walikuwepo waliohit na walitamba kweli kweli, muda wako unaokuwa nao tumia vizuri usianze kudharau watu, ninachoamini ni kwamba ukiwepo kwenye nafasi yako itumie vizuri hakikisha kwamba hugombani na watu kesho na kesho kutwa wakashindwa kukusapoti''

Niambie mdau unampa point ngapi Shilole kwenye hili dondosha comment yako hapo chini 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags