Shangazi: Suleman aliogopa kwenda safarini

Shangazi: Suleman aliogopa kwenda safarini

Ikiwa familia zinaendelea kuomboleza kuwapoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, Shangazi yake Suleman Dawood, ambaye alikuwa kwenye nyambizi ya Titan na baba yake Shahzada, anasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa anasitasita kuhusu safari ya kwenda kuona ajali ya Titanic.

Akizungumza na NBC News, Azmeh Dawood, alisema Suleman alimwambia kwamba alihisi kuogopa kuhusu safari hiyo, lakini alitaka kumfurahisha baba yake.

Walipanda nyambizi hiyo Jumapili iliyopita, ambayo ilikuwa Siku ya Akina Baba huko Amerika Kaskazini.

“Siamini kilichotokea, Ni hali ya kushangaza Ninahisi kama nimenaswa katika hali hatari sana, na muda unayoyoma, lakini haujui utafanya nini kujinusuru, Mimi binafsi napata tabu kupumua nikiwafikiria” alisema Shangazi yake Suleman

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags