Shamsa Ford alia na TANESCO,  Awaza marejesho

Shamsa Ford alia na TANESCO, Awaza marejesho

Ikiwa tatizo la umeme linaendelea kuwatesa baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali, huku baadhi ya ‘mastaa’ wakilalamika kuhusiana na mgao huo.

Muigizaji wa filamu nchini Shamsa Ford ameyatoa ya moyoni kwa kuliomba Shirila la Umeme Tanzania (TANESCO) kumaliza tatizo hilo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa muigizaji huyo ameshusha ujumbe ukieleza,

“TANESCO tunawaomba tupo chini ya miguu yenu huu mgao wa umeme uishe jamani, mnatuumiza mnoo. Sisi vijana tunapambana na maisha lakini umeme unatukwamisha.

Biashara zinasimama kwa sababu ya umeme wengine biashara tunafunga saa 4 usiku lakini kwa sababu ya umeme itabidi ufunge saa 12 jioni.

TANESCO wengine tuna marejesho ya kausha damu tutashindwa kupeleka marejesho yao tufunge viduka, yaani ukiwa ‘ofisini’ umeme hakuna biashara zinasimama na ukirudi nyumbani umeme hakuna vile vinyama tunavyohifadhi kwa fridge vimeharibika.

 

 “Mnatuumiza mnoo, huo mgao utaisha lini au ndo maisha yetu”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags