Shamsa agoma uke wenza

Shamsa agoma uke wenza

Mwigizaji Shamsa Ford amesema watu wamuache kwa sasa ametulia kwenye ndoa yake na hayupo tayari mume wake ambaye ni msanii mwenzake Hussein Lugendo 'Mlilo' aoe mke wa pili.

Shamsa amesema hayo baada ya baadhi ya watu kumsema anatamba sana na ndoa yake kwenye mitandao ya kijamii na kumposti kila wakati mume wake, hivyo ameambiwa awe makini ataongezewa mwanamke na mume wake huyo.

“Watu wanasema tu, unafikiri kuongezewa mke ni mchezo? Sasa nisitambe na ndoa yangu wanataka nitambe na nani? Huu ni wakati wangu, acha nimpostiposti au tujipostiposti na kwanza sidhani kama ndiyo sababu itamfanya mume wangu kutaka kuoa mke wa pili, na endapo mwanamke yeyote akifuatwa na mume wangu, basi ajue kabisa anadanganywa kwani mimi ndiye mwenye nyumba na nitakuwa peke yangu labda hadi nitake.

“Kwanza mume wangu ananipenda, ni mtulivu na hana mtu mwingine zaidi yangu. Kwake niko peke yangu, ninajiamini kwa sababu napendwa,”  alisema Shamsa.

Shamsa aliongeza kusema: “Mwanaume anaongeza mke mwingine kwa sababu fulani, aidha mwanamke jeuri, hawezi kumshauri mumewe hata jambo la maana hata siku moja na kukiwa hakuna maendeleo, hapo ni lazima atakuongezea mwenzako. Kama wanavyosema mwanamke jeuri mwongezee mwenzie.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags